HIS LIFE

 

Jina: Raphael Joachim Lyela
Nimeoa mke mmoja anaitwa Angela mwaka 29.05.2010. Mtoto wa tatu kati ya sita katika familia ya Mzee Joachim Lyela, nimezaliwa miaka 33 iliyopita na mama yangu alifariki nikiwa na miaka 10 kule Mwanza. Nilisoma elimu ya msingi shule ya Mabatini Mwanza mpaka darasa la pili ambalo sikumaliza, ugumu wa maisha ukanifanya nitoroke nyumbani na kwenda Sumbawanga nilikomaliza elimu ya msingi mwaka 1995,nikajiunga elimu ya secondari katika shule ya Kipoke Tukuyu-Mbeya mwaka 1997, nikahamia shule ya Lutengano mpaka mwaka 1999 nikiwa kidato cha tatu yakatokea matatizo yaliyonifanya niache shule na nikarudi tena shule mwaka 2001 katika shule ya Iyunga na nikamaliza kidato cha nne mwaka 2002. Nikapata Division 3 na kuchanguliwa katika shule ya Kigonsera-Ruvuma kwa mchepuo wa HGL, nikasoma muhula mmoja na kisha nikahamia shule ya sekondari ya Sangu-Mbeya nilipohitimu mwaka 2004 na kupata Division 1.8 na kuchaguliwa chuo kikuu Mzumbe mwaka 2005 na kuhitimu shahada yangu ya kwanza mwaka 2008. Nikapata kazi katika shirika la Compassion International Tanzania kuanzia 2008 mpaka leo hii.

Kutokana na ugumu wa maisha nilijaribu kujiua kwa kuruka toka kwenye treni ikiwa katika mwendo wake mwaka 1993 katika eneo la Urambo lakini sikufanikiwa kufa na ninaishi mpaka hivi leo. Nimesoma kwa kuunga unga mpaka kumaliza chuo kikuu.Nimefanya kazi na kampuni ya Celtel kama Customer care.

Mwaka 2005, mimi pamoja na rafiki zangu wawili, Biton na Maulid tulianzisha kituo chetu cha tuisheni pale Mwenge nyuma ya Nakiete Pharmacy mwaka 2005 kwa jina la Mapambano Remix Academic Center na nilikuwa nafundisha HGL.

Nilipata wazo la kuwatumikia Vijana mwaka 2003 baada ya kuhudhuria mkutano wa Vijana uliofanyika bungeni Dodoma chini ya Youth of the United Nation Association of Tanzania(YUNA), niliona fursa niliyorudi nayo Mbeya nilikokuwa nakaa kwa kipindi hicho.

Nilipookoka ndipo nilipoanza rasmi kutuma jumbe zenye neno la Mungu mwaka 2007 kwa Vijana 24, kisha nikapata wazo la Mindset Upgrade mwaka 2008 na kisha kuzaliwa rasmi kwa huduma inayofahamika sasa kama YKM iliyoanza rasmi mwaka 2012. Nimekuwa Mchungaji wa Vijana katika kanisa la TAG Miyuji-Dodoma-Capital Christian Center toka 2011 mpaka sasa. Kabla ya hapo nikiwa Arusha nilikuwa katibu wa Vijana katika kanisa la EAGT Elerai, mwenyekiti wa timu ya kusifu na kuabudu.

Nimeandika vitabu vingi sana vya Vijana ambavyo bado havijatoka, nimetoa kitabu cha KUISHI MAISHA YA IMANI KATIKA ULIMWENGU USIOAMINI mwaka 2009, ninarusha kipindi cha Vijana katika Radio Uzima FM-Dodoma toka mwaka 2012, ni mtunzi wa nyimbo na mwimbaji wa nyimbo za kumbwabudu Mungu.