Maamuzi ni msimamo wa ndani au commitment, unapofanya maamuzi usifikiri unafanya jambo jepesi au rahisi, matokeo ya maamuzi unayofanya yanaweza kukuharibia kabisa maisha yako au yakakuletea matokeo mazuri ya maisha yako, usikurupuke, maamuzi ni vita na ndio maana ulipoamua kufanya maamuzi fulani ndipo ulipowajua hata maadui zako eg, kuokoka, kubadili tabia


Maamuzi ni msimamo wa ndani

 Kama una amini Mungu anayathamini maisha yako basi ujue pia kuwa anajali maamuzi yako kwahiyo fahamu kuwa ipo nafasi ya Mungu katika maamuzi yako, usiingie kwenye mtego wa kuamua peke yako, ni bora usiende vitani kama huna hakika Mungu yuko nawe, tambua nafasi ya Neno lake, 1 Falme 11:26-39, Mithali 16:1-4

Mungu anayathamini maisha yako

Ipo nafasi ya maombi kwa maamuzi yaliyo na matokeo mazuri, maombi kwa Mungu,muombe Mungu ili akusaidie kuyathibitisha maamuzi yako, mkabidhi Bwana njia zako ili ayathibitishe mawazo yako,kumbuka maamuzi yanatoka ndani ya mawazo au fikra zako, Zaburi 19:14

Ipo nafasi ya maombi kwa maamuzi yaliyo na matokeo mazuri

Maamuzi mazuri yanahitaji muda wa kujipanga eg Rehoboam alihitaji siku 3, hii inakupa fursa ya kujiridhisha juu maamuzi hayo ikiwa ni pamoja na kutafuta ushauri na kuyaombea maamuzi hayo,

Maamuzi mazuri yanahitaji muda

Unahitaji hekima ya kukuongoza kufanya maamuzi hayo na namna ya kuyasema au kuyawasilisha, unaweza ukawa na maamuzi mazuri kabisa lakini ukishindwa kujua the how au namna ya kuyafanya au kuyasema au kuyachukulia hatua utafanya vibaya-1 Falme 12:1-7,12-18

hekima ya kukuongoza kufanya maamuzi

Hakikisha una ufahamu wa kutosha na uliosahihi wa jambo unalotaka kulifanyia maamuzi, eg, kama unataka kufanya biashara au unataka kuwekeza fanya utafiti wa kutosha, uliza taarifa na upate habari zitakazoweza kukusaidia kufanya maamuzi hayo, usikurupuke  kuamua kwa haraka ingawa yapo maamuzi ya kuamua kwa haraka kutegemeana na mazingira na wakati

ufahamu wa kutosha na uliosahihi

Quotes by Raphael JL:Usimheshimu mtu baada ya kumdharau,maana wengi kwa kufanya hivo wamejinyima fursa zilizokuwa ndani ya waliowadharau na wakagundua kuwa wanawahitaji badae,kwani dharau ni ufahari?
:Jesus Up-YKM!

Usimheshimu mtu baada ya kumdharau

Quotes by Raphael JL:Kuikimbia tamaa bila kujua unakokimbilia ni sawa na kutaka kucheka huku unalia,usipojua unakokimbilia unapofukuzwa na adui utaishia kuingia kwa rafiki wa adui ukadhani uko salama kwa muda.
:Jesus Up-YKM!

Kuikimbia tamaa

Quotes by Raphael JL:Kumuomba Mungu abariki kazi za mikono yako na huku mikono yako haina kazi inafanya ni sawa na kuomba upate usingizi wakati umeshalala kitambo.
:Jesus Up-YKM!

Mungu abariki kazi za mikono

Quotes by Raphael JL:Ukitaka ujibiwe vizuri au upate jibu sahihi basi jifunze kuuliza swali vizuri na kwa usahihi. :Jesus Up-YKM!

Ukitaka ujibiwe vizuri

Quotes by Raphael JL:A good leader doesnt use people but build and empower them for one mission and not selfishness. Be that leader. :Jesus Up-YKM!

A good leader